Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa
kifungu Namba 6 Kifungu kidogo cha 2 (b) cha Sheria ya Bandari namba 17 ya
mwaka 2004 kinachompa mamlaka ya kuvunja na kuteua wajumbe wa bodi.
Sitta alitangaza uteuzi huo jana
jijini Tanga wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Tanga na baadaye
kuzungumza na wafanyakazi waliokusanyika katika uwanja wa Baraka na kusisitiza
kuwa mabadiliko hayo yametokana na vitendo vya uonevu alivyokuta vikiendelea
kufanywa ndani ya TPA.
Wajumbe wapya walioteuliwa ni pamoja
na Mhadhiri wa Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Tulia Akson; Mhandisi
wa Ujenzi, Musa Ally Nyamsingwa; Mtaalam wa Manunuzi na Mjumbe wa Bodi ya
Posta, Donata Mugassa na Mkurugenzi Mkuu mstaafu wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Nishati na Maji (Ewura), Haruna Masebu.
Wengine ni Mhandisi wa Bodi ya
Wahandisi Tanzania, Gema Modu; Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam,
Francis Michael; Mkurugenzi wa Mipango NSSF, Crescentius Magori na aliyekuwa
Mkurugenzi wa Masoko wa TPA, Flavian Kinunda.
Dk. Michael na Akson walikuwa
wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, ambalo Sitta alikuwa mwenyekiti wake.
“Uteuzi huu unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia leo Juni 2, mwaka huu na lengo la uteuzi wa wajumbe hawa ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi ndani ya wa Mamlaka na kwa nafasi ya Mwenyekiti mpya wa Bodi nasubiri uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete kwani ndiye mwenye mamlaka hiyo kisheria,” alisema.
Dk. Mwakyembe aliteua bodi ya TPA
Novemba 6, 2012.
Mwakyembe aliwateua Dk. Jabir Kuwe
Bakari, John Ulanga, Caroline Temu, Jaffer Machano, Dk. Hildebrand Shayo, Said
Salum Sauko, Mhandisi Julius Mamiro na Asha Nasoro.
Sambamba na hatua hiyo Waziri Sitta
aliziagiza taasisi zote zilizo chini ya wizara ya Uchukuzi ikiwamo Mamlaka ya
Hali ya Hewa, Mamlaka ya Usimamizi wa Anga, Reli na Bandari kuhakikisha
wanabuni mifumo mipya ya motisha ndani ya mamlaka zao ili wafanyakazi wa ngazi
za chini wajione ni sehemu ya mamlaka husika.
0 comments:
Post a Comment