Image
Image

Taifa Stars sasa iko fiti kutua Ethiopia kuikabili Misri.


Kundi la kwanza la kikosi cha timu ya taifa TAIFA STARS litaondoka nchini Alhamisi kwenda Ethiopia kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wake dhidi ya Misri juni 14 wakati kundi la pili litaondoka ijumaa kwenda Rwanda kucheza mchezo maalum wa kumbukumbu ya mauaji ya kimbari utakaochezwa juni 6 nchini humo.
Stars ambayo iliingia kambini jijini Dar es Salaam kwa awamu mbili imegawanywa katika makundi mawili ambapo kundi la kwanza lenye wachezaji 23 linaloundwa na wachezaji wanaocheza ndani na nje ya nchi litaondoka Alhamisi kwenda kujichimbia nchini Ethiopia kujiwinda dhidi ya timu ya mafarao wa misri katika mchezo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali za Afrika-Afcon utakaochezwa jijini Alexadria, Misri.
Wakati kundi la kwanza litaongozwa na kocha mkuu mholanzi Mart Nooij atakayesaidiwa na Mecky Mexime, kundi la pili litakaloondoka nchini ijumaa litakuwa chini ya kocha Salum mayanga na baada ya kurejea nchini baadhi ya wachezaji watajumuishwa na wenzao waliokuwa misri kwa ajili ya mchezo wa kusaka tiketi ya kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani-chan dhidi ya uganda THE CRANES utakaochezwa juni 20 kwenye uwanja wa amaan kisiwani Zanzibar..
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment