Mratibu wa wa bball kitaa karaban ikarabani amesema pambano hilo ambalo linatarajiwa
kuvuta hisia za maelfu ya mashabiki kutoka wilaya zote za jiji la Dar es salaam
yaani kinondoni, temeke na ilala litafanyika katika uwanja wa bball kitaa Park,
uliopo karibu na ukumbi maarufu wa
Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Karabani pia alizitaja kanda zingine ambazo
zitashiriki katika michuano hiyo mwezi julai kuwa, ni mabingwa watetezi kanda
ya nne ya mashariki inayoundwa na wachezaji kutoka temeke na mbagala kanda ya kwanza ya
Mashariki, kanda ya tatu ya mashariki, kanda ya pili
ya magharibi, kanda ya tatu ya magharibi na kanda ya kanda ya nne ya magharibi.
Mshindi wa michuano hii ya nnen gazi ya kanda atakabidhiwa kitita cha shilingi
milioni 5.
Kwa upande wake, meneja bidhaa wa coca-cola nchini
maurice njowoka amsema kuwa kampuni ya coca-cola kupitai kinywaji cha sprite
imejiona ni yenye heshima kubwa mara baada ya kupewa fursa ya kudhamini
michuano hiyo nchini na kuahidi kuwa kampuni yake kuendelea kutoa ushirikiano
wa bega kwa bega kuhakikisha kuwa mchezo huu unazidi kusonga mbele.
0 comments:
Post a Comment