Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa
marekani mjini Bujumbura, imemtaka Rais Nkurunziza azingatie upya azma yake hiyo ili kuunusuru mkataba wa Arusha.
Vyama vya upinzani na jumuiya za
kiraia nchini humo vinasema mpango wa kiongozi huyo unakiuka katiba inayosisitiza
juu ya mihula miwili na pia makubaliano ya amani ya Arusha.
Rais Nkurunziza anadai muhula wa
kwanza alichaguliwa na bunge na sio umma.
Uchaguzi wa bunge nchini Burundi
unatarajiwa kufanyika tarehe 5 mwezi huu ukifuatiwa na wa rais juni 26.
Taarifa ya marekani imetolewa baaada ya mkutano wa
kilele wa viongozi wa kanda hiyo kuhusu Burundi, uliofanyika Dar es Salaam
mwishoni mwa juma kutaka uchaguzi uahirishwe hadi katikati ya mwezi julai.
Marekani pia imejiunga na wale
wanaotoa wito kutoka uchaguzi uahirishwe.
0 comments:
Post a Comment