MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe amesema anategemea kufanya
vizuri zaidi katika michuano ijayo ya Kagame kuisaidia timu kuchukua
taji katika michuano hiyo itakayofanyika nchini kuanzia mwezi ujao.
Tambwe, ambaye aliwahi kufanya vizuri katika michuano hiyo
iliyofanyika Sudan miaka miwili iliyopita kwa kuibuka mfungaji bora,
aliliambia gazeti hili kuwa anajipanga kufanya vizuri zaidi.
Mchezaji huyo aliibuliwa na Simba katika michuano hiyo wakati
akiichezea Vital’O ya Burundi iliyochukua ubingwa wakati huo, kutokana
na kuisaidia timu yake kwa kiasi kikubwa na kufanya vizuri.
“Ni kazi yangu kuhakikisha nafanya vizuri katika timu, ndio maana
kila siku najituma kuwezesha timu yangu kushinda, na kwa sasa najipanga
kwa ajili ya Kagame nikitegemea kufanya makubwa zaidi,” alisema.
Alisema kwa mbinu ambazo aliwahi kuzionesha Sudan akiwa na timu yake ya zamani atazitumia kuipa ushindi Yanga.
Mchezaji huyo aliyejiunga na Yanga msimu uliopita, ni miongoni mwa
wachezaji waliokisaidia kikosi hicho cha Jangwani kuchukua taji la
ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita.
Aliahidi kufanya vizuri zaidi ikiwezekana kujitahidi kufungwa na kuwa mfungaji bora katika michuano yote ijayo.
Mrundi huyo ni kati ya wachezaji tegemeo wa kikosi cha Yanga
wanaotarajiwa kushuka dimbani kesho katika mchezo wa kirafiki dhidi ya
Sports Villa ya Uganda, mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment