SERIKALI imeitaka Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA); kulinda afya za Watanzania, kudhibiti soko la bidhaa bandia.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu Kiongozi,Sefue Ombeni,wakati wa kuzungumza na
wafanyakazi wa TFDA katika, Wiki ya Maonyesho ya Utumishi wa Umma.
Ombeni
amesema TFDA ni chombo ambacho kimepewa mamlaka na serikali kwa
kudhibiti na kusimamia afya za Watanzania; hivyo hakuna budi kudhibiti
mianya ambayo inapitisha bidhaa ambazo hazina ubora.
"Serikali ipo pamoja na TFDA mwendeleze majukumu yenu kwa kusimamia misingi ya kazi yenu," alisema Sefue.
Kwa
upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiti Silo,amesema TFDA ni Taasisi
iliyo chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, yenye jukumu la
kudhibiti usalama na ubora wa chakula; dawa na vipodozi na vifaa tiba.
Silo
amesema mamlaka hiyo imeundwa chini ya sheria ya chakula dawa na
vipodozi ya mwaka 2003 na mwaka 2013 imetimiza miaka 10 na mamlaka
inatimiza majukumu yake kwa kuzingatia sheria.
Kuhusu mafanikio
katika kipindi cha miaka 10 TFDA imefanikiwa kujenga ofisi ya ghorofa
tatu lililozinduliwa mwaka 2008 na aliyekuwa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar; Dkt. Amani Abeid Karume.
Aidha,amesema
katika kipindi cha miaka kumi TFDA imefanikiwa kuhakiki usalama, ubora
na ufanisi wa bidhaa, chakula, dawa, vipodozi na vifaa tiba.
"Katika
kipindi hicho jumla ya bidhaa 19,635 zimesajiliwa kama ifuatavyo
vyakula 5,918,dawa 4,782, vipodozi 3,968 na vifaa tiba 4,967.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment