Utekelezaji wa mpango huo umeanza
kwa baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo kutoka nchini na nje ya nchi kuanza safari ya kupanda mlima huo na kwamba
kampuni inatarajia kukusanya dola za Marekani milioni nane kutokana na program
hiyo.
Akizungumza katika lango la Machame
la kuingilia mlima Kilimanjaro ambako wafanyakazi hao walianzia kuupanda mlima
huo, Kaimu Mhifadhi wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro CHARLES NGEDO amesema kwa
tanzania licha ya kuwanufaisha wanafunzi wanaolengwa pia ni njia pekee ya kuutangaza mlima huo
kimataifa.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya
ACACIA inayomiliki migodi ya Bulyankulu, Buzwagi na North Mara BRAG GORDON na
wafanyakazi walio kwenye safari ya kupanda mlima wamesema wanaamini kuwa zoezi
hilo ambalo litakuwa endelevu litawanufaisha watoto wengi hususani wale
wanaotoka kwenye familia duni.
0 comments:
Post a Comment