Nyongeza hiyo imetangazwa na Waziri
wa Fedha,SAADA MKUYA SALUM kufuatia kilio cha wabunge wakati wakijadili hali ya
uchumi wa taifa kwa mwaka 2014 na mwelekeo wa mpango wa maendeleo na bajeti ya
serikali kwa mwaka 2015/2016.
Wame sema kiwango cha awali
kilichokuwa kimetangazwa na Waziri huyo cha k uongeza pensheni ya wazee wasta
afu kutoka Shilingi Elfu-50 hadi
Shilingi Elfu- 85 kilikuwa kidogo
mno kulingana na mchango wao kwa taifa
lao.
Bunge baadaye lilipitisha bajeti
hiyo ya serikali ambayo ni zaidi ya Shilingi TRILIONI 22.4.
Mapema ilitangazwa Bungeni kwamba
Tanzania na Zambia zimekubaliana kurekebisha sheria zao za kuendesha Mamlaka ya
Reli ya Tanzania na Zambia TAZARA ili kuwezesha uendeshaji wa reli hiyo kwa
njia ya ubia wa sekta binafsi na umma kwa kuvutia wawekezaji binafsi.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri ADAM
MALIMA wakati akielezea matatizo ya reli
hiyo inayohitaji kiasi cha dola za
Marekani milioni 100 ili kuleta uf anisi katika uendeshaji wa reli hiyo kutoka kituo cha Kapiri Mposhi, Zambia
hadi Dar es Salaam, Tanzania.
0 comments:
Post a Comment