Image
Image

SERIKALI yawatoa wasiwasi wananchi ambao hawajaandikishwa kwenye daftari la wapiga kura Arusha.


Serikali Mkoani  Arusha imewataka  wananchi   ambao  bado  hawaj ajiandikisha  kwenye  Daftari  la Kudumu la  W apiga Kura  kutokuwa  na  wa siwasi  kwani ikibidi  muda utaongezwa  wote wenye  sifa waandikishwe.
Akizungumza  baada  ya   kutembelea  baadhi  ya  vituo,  Mkuu  wa Mkoa  wa  Arusha,Bwana DAUD I  NT I BENDA  amesema   matatizo yaliyojitokeza     yanashughulikiwa   kushuhulikiwa  na  zoezi  linaendelea   vizuri  na  halitasimamishwa  hadi   wananchi wwote  waandikishwe .
Baadhi  ya Mawakala   wanaoendes ha  zoezi hilo   wamesema  kwa  tatizo  la  upungufu  wa mashine limepungua,lakini  bado lipo tatizo la  baadhi  ya  watu   wasio  wakazi  wa maeneo husika  kuvamia  katika  vituo jambo linal osababisha  msongamano  usio  wa  lazima .
Nao  baadhi  ya  wananchi   wamesema  kumeibuka  kundi  la  madalali    wanaowahi  kwenye  vituo  na   kushika  nafasi  na  kuwauzia  watu  wenye  haraka  kati  ya  Shilingi  E lifu- kumi hadi  Shilingi  Elfu-15   na wameiomba  Serikali   kukomesha  tabia  hiyo .
Zoezi la uandikishaji   wa  wananchi  katika  Daftari la  Kudumu   la Wapiga  Kura  kwa  kutumia  mashine  za  BVR  limekuwa  na  heka  heka  kubwa  katika  Mkoa  wa  Arusha  ambazo  kwa  asilimia  kubwa  zinadaiwa   kuchochewa  na  masuala  ya  k siasa .
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment