Image
Image

TFF imemtangaza Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa na Kocha Mkuu wa Mafunzo ya Zanzibar,Hemed Morocco

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limemtangaza Kocha Msaidizi wa Yanga, Charles Mkwasa na Kocha Mkuu wa Mafunzo ya Zanzibar, Hemed Morocco kufundisha Taifa Stars badala ya Mart Nooij na Salum Mayanga waliofukuzwa.
Makocha hao wamepewa jukumu la kuiongoza Stars katika mechi ya marudiano dhidi ya Uganda itakayochezwa Julai 4, mwaka huu nchini humo, na michuano ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017.
Uteuzi huo umekuja siku chache baada ya TFF kutangaza kumfukuza kazi Nooij kwa kushindwa kufanya vizuri katika michezo mbalimbali ya kimataifa, ikiwamo kupoteza mechi tano za karibuni.
Akitangaza makocha hao jana, Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema kabla ya kumteua Mkwasa, alifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji kupata baraka zake kwa vile bado ana mkataba na klabu hiyo ya Jangwani inayoshikilia ubingwa wa Tanzania Bara.
“TFF inatambua kwamba Mkwasa bado ni kocha wa Yanga na ataendelea kuifundisha klabu hiyo, na wakati tutakapomhitaji ataendelea kuwa nasi kwa kipindi hiki kifupi,” alieleza Malinzi aliyemuajiri Nooij, Aprili 25, mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili.
Alisema tayari ameshaandika barua serikalini kuomba mshahara aliokuwa akilipwa Nooij, nyumba na gari apewe Mkwasa hivyo wanasubiri majibu kutoka huko.
Malinzi alisema uteuzi wa makocha hao umezingatia uwezo na leseni walizonazo kwani ni makocha wazalendo watano pekee ambao wana leseni A zinazotambulika Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na la Afrika (CAF).
Makocha wazalendo wenye leseni hizo ni Mkwasa, Morocco, Abdul Mingange, Jamhuri Kihwelu na Juma Mwambusi.
Kwa mujibu wa Malinzi, Mkwasa na msaidizi wake watakuwa na jukumu la kuteua benchi jipya la ufundi ambalo watalipeleka kwenye Kamati ya Utendaji. Pia Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Msafiri Mgoyi alitangazwa kuwa Mratibu wa timu ya Taifa.
Katika hatua nyingine, Malinzi alisema fedha za ada ya Dola za Marekani 2,000 (zaidi ya Sh milioni nne) zitakazotolewa na klabu kwa usajili wa kila mchezaji wa kigeni zitaingizwa katika akaunti maalumu kwa ajili ya kusaidia Mfuko wa Maendeleo ya Soka la Vijana na Wanawake.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment