Image
Image

Ufahamu ugonjwa wa pumu na jinsi watu wengi walivyo hatarini.


Mtu mwenye pumu huwa na mcharuko uvimbe sugu mwilini kwenye mirija yake ya kupitishia hewa (bronchioles tubes) hali ambayo husababisha kuvimba kwa kuta za mirija hii na kuwa na ute mzito hivyo kupungua kwa njia ya kupitishia hewa. Hali ambayo humfanya muathirika kushindwa kuvuta na kutoa hewa nje na hivyo kupumua kwa shida sana. Tatizo hili linaweza kudumu kwa muda mfupi au mrefu kiasi cha kuhitaji tiba ili kumuwezesha mgonjwa kupata nafuu.
Kutokana na kuwepo kwa msuguano na uzuiaji wa kupitisha hewa wakati wa kupumua hewa nje, pumu hujulikana pia kama obstructive lung disease .
Mtu aliye na pumu huwa na kipindi ambacho hawi na tatizo la pumu mpaka pale mwili unapochokozwa na kuingia katika hali hiyo. Wakati huo hote cha maisha yake kinachotokea ni kutulia tu mpaka pale inapotekea uchokozi mwilini.
Pumu inaweza kugawanywa katika makundi mawili, iko pumu ya ghafla ijulikanayo kitabibu kama Acute asthma. Wagonjwa wanaopatwa na kundi hili la pumu huwa na hali ya kawaida katika njia zao za hewa isiyobadilika wakati wa shambulio na usio wa shambulio.
Kundi nyingine ni Pumu sugu (Chronic Asthma). Kundi hili la pumu huwa na tabia ya kuwa na njia nyembamba za kupitisha hewa na kadiri jinsi mgonjwa anavyoendelea kupata matukio zaidi ya pumu njiaza hewa huzidi kuwa nyembamba na kusinyaa zaidi.
Aina za pumu
Bila kujalisha mgonjwa anaingia katika kundi gani, ugonjwa wa pumu unaweza kugawanywa katika aina kuu nne, ambazo ni inayobadilika, isiyobadilika, ya mazoezi na inayosababishwa na kazi.
Pumu inayobadilika (brittle asthma): Kulingana na tabia ya kujirudia rudia kwa matukio ya ugonjwa huu na madhara yake kwa mgonjwa, aina hii ya pumu inaweza kugawanywa zaidi katika aina nyingine mbili.
Aina ya kwanza ya pumu inayobadilika (type 1 brittle asthma) ni pumu yenye tabia ya kuwa na matukio na mashambulizi ya kubadilika kila mara japokuwa mgonjwa anaweza kuwa anapata matibabu kadhaa.
Aina ya pili ya pumu inayobadilika (type 2 brittle asthma) ni pumu ambayo mgonjwa anatokea kupata shambulizi la ghafla (asthmatic attack) wakati hapo awali ugonjwa wake uliweza kuthibitiwa kwa matibabu.
Pumu hatari isiyobadilika (status asthmaticus): Hii ni aina ya pumu iliyo hatari zaidi kwa mgonjwa. Pamoja na matumizi ya dawa kadhaa, zikiwemo vitanua njia za hewa (bronchodilators) na vipoza mcharuko mwili (steroids), mgonjwa wa aina hii ya pumu anaweza asipate nafuu ya haraka na anaweza kupoteza maisha.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment