Image
Image

Elimu ya hedhi itolewe kuanzia ngazi ya shule za msingi nchini.



Mei 28, mwaka huu, kwa mara ya kwanza, Tanzania iliungana na na nchi nyingine duniani kuadhimisha siku ya hedhi ambapo jamii inaelimishwa kuhusiana na jambo hilo ambalo ni la kawaida katika mfumo wao wa maisha, kila baada ya wastani wa siku 28. Ofisa Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Madina Kemilembe alizindua kwa mara ya kwanza nchini maadhimisho hayo katika viwanja vya mnazi mmoja.
Maadhimisho ya mwaka huu yalifanyika kwa kauli mbiu kwamba “usisite kuzungumzia hedhi,” ikiwa ni sehemu ya kuihamasisha jamii kutambua na kuelewe umuhimu wa elimu kwa jambo hilo.
Kemilembe anasema nchi yetu inatambua umuhimu wa siku hii na inaunga mkono jitihada za umoja wa mataifa kwa kuwa bado jamii iko nyuma inaona jambo la ajabu kutoa elimu ya hedhi kwa watoto wao .
Kemilembe alizungumzia changamoto zinazo wakuta wanafunzi wa kike na kukwamisha mahudhurio yao katika masomo kuwa ni unyanyapaa wanaopata kutoka kwa wanafunzi wa kiume kutokana na kutokuwa na elimu ya swala hilo na kuona ni uchafu.
Anaeleza kuwa ukienda vijijini utakuta wanafunzi hawajui jinsi ya kujihifadhi kipindi wanapokuwa kwenye hedhi na kusababisha kila mwezi kukosa masomo kwa siku tano jambo linalosababisha kurudi nyuma kielimu.
Kemilembe anasema alienda vijijini akakuta watoto wanajihifadhi kwa kutumia ugali. Anafafanua kwamba baada ya kuupika wanauweka kwa siku tatu na baadaye wanaukata na kuutumia kama kifaa cha kujihifadhi nyakati za hedhi. “Ni vitu vya ajabu! Wengine wanatumia vitambaa ambavyo siyo salama,” anasema Kemilembe akifafanua:
“Tukiwauliza kinamama ni wangapi wenye uwezo wa kuwanunulia wanawe pea saba za kanga ili atumie kujisitiri wakati wa hedhi, wanasema hawawezi,” anasema huku akionya kwamba kutumia vitu ambavyo siyo safi au ambavyo vinaweza kusababisha uambukizo ni hatari kwa sababu vinaweza kuwa chanzo cha saratani ya kizazi.
Changamoto nyingine kwa mtoto wa kike, anazitaja kuwa ni kukosekana kwa maji safi na salama, vyoo, pedi na mahali pa kubadilishia nguo wakati wako kwenye hedhi.
Kuwepo kwa matatizo hayo, anasema ndiyo sababu za mtoto wa kike kutohudhuria vyema masomo wakati yupo kwenye hedhi na matokeo yake kurudi nyuma kielimu.
Kemilembe anasema Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamekubaliana kuandaa na kusimamia sera inayoondoa vikwazo kwa watoto wa kike katika masomo yao.
“Nawashukuru wadau kutoka Water Aid, Shirika la Maendeleo la Uholanzi (SNV), Kasole Secrets pamoja na wengine kwa kuisaidia serikali kuandaa mazingira rafiki kwa watoto hawa. Wamewajengea vyumba vya kubadilishia na kuhakikisha upatikanaji wa pedi kwa baadhi ya shule,” anasema Kemilembe.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment