Ofisa wa Idara ya Daftari la Wapiga Kura katika tume hiyo Bwana
JAMBIA KOBELSK amesema mashine hizo ambazo ni mpya zinafanya kazi kwa ufanisi
lakini kuna baadhi ya maeneo zinachagua hali ya hewa.
Hali hiyo inasababisha zoezi hilo kwenda taratibu hatua ambayo
imeanza kufanyiwa kazi ili azma iliyowekwa ya kukamilisha mchakato huo iweze
kufikiwa.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Bwana SALIM CHIMA amewataka
waandikishaji kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi kwa sababu endapo watafanya
zoezi hilo pasipo kuzingatia kanuni wanaweza kusababisha machafuko katika
uchaguzi uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa zoezi hilo mkoni Tanga Bwana LEWIS
KALINJUNA amesema kikubwa zaidi ni jinsi gani ya kujifunza matumizi ya mashine
za kielektroniki ili kurahisisha zoezi hilo liweze kufanywa kwa ufanisi.
0 comments:
Post a Comment