Kitoto hicho kichanga cha kiume kinachokadiriwa kuwa na miezi tisa
kilitupwa chooni nyumbani kwa jirani ambaye ni mchungaji wa kanisa la
Pentekoste.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema mwanamke huyo ambaye ni mama mwenye
watoto wawili amebainika kufanya kitendo hicho nyakati za usiku baada ya
mwenyewe kuanza kueleza watu kwamba kuna mwanamke aliyetupa chooni kitoto
kichanga kilichosikika kikilia usiku kucha.
Polisi walipokagua chooni walibaini kuwepo kwa kichanga hicho kilichokuwa
kimefungwa kwenye mifuko ya nailoni,maarufu kama Rambo,huku Kikiwa tayari
kimekufa.
0 comments:
Post a Comment