Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala jijini Dar es
Salaam wameiomba kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za jamii kwenda chuoni
hapo ili kuwasikiliza na kutatua kero zinazowakabili wanafunzi wanaosoma chuoni
hapo.
Ombi hilo limekuja baada ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
DR. SHUKURU KAWAMBWA kudaiwa kushindwa kuutatua mgogoro huo huku wanafunzi hao
wakipata mateso makubwa.
Aidha baadhi ya wanafunzi hao wamekwenda mbali zaidi kutoa madai
ya kutambuliwa kama wanafunzi kutoka nje ya nchi huku serikali ikitambua kuwa
si kweli kutokana na kupata mikopo ya elimu ya juu kama wanafunzi wengine
wazawa wanavyopata lakini pia wakataka ufafanuzi wa baadhi ya masuala kutoka
serikalini.
Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala cha jijini Dar es salaam kimekuwa
kikikumbwa na migogoro ya mara kwa mara kati ya chuo hicho na wanafunzi.
0 comments:
Post a Comment