Tamko hilo limetolewa na mkutano mkuu maalum uliyoshirikishwa
vyama tisa kutoka kanda zote kufuatia
hatua ya makampuni ya mawakala wa utalii nchini kupuuza maagizo ya Wizara ya
Mali asili na Utalii mwaka 2009 kuongeza
viwango na kuyafanya makampuni hayo kulipa wastani wa dola tano hadi 10.
Mwenyekiti wa Chama cha Waongoza Watalii Mkoani Kilimanjaro Bwana
RESPICIUS BAITWA amesema makampuni hayo
yamepuuza kulipa kwa siku viwango hivyo vya wastani wa dola 10, 15 hadi 20 kwa wapagazi, wapishi na waongoza watalii
kwa siku.
Naye Katibu wa Muungano wa
Vyama vya Wapagazi nchini Bwana MUGABO MAGOTO ameitupia lawama serikali kwa kutoyachukulia hatua za kisheria
baadhi ya makampuni ya uwakala wa utalii yanayofanya biashara hiyo bila kibali
na kuliibia taifa.
0 comments:
Post a Comment