Kwa mujibu wa ripoti hiyo,
Crispus Kiyonga alikutana na Dina Kawar na kujadiliana naye masuala mbalimbali
ya Kongo DRC, kubwa zaidi ikiwa ni suala la magendo ya dhahabu ya Kongo.
Katika
mazungumzo hayo Waziri wa Ulinzi wa Uganda amesema kuwa, Kampala inafanya kila
juhudi kupambana na magendo ya dhahabu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Amesema kuwa, kutodhibitiwa vyanzo vya utajiri wa maliasili mashariki mwa Kongo
DRC, kunatoa mwanya kwa makundi ya wabeba silaha kutumia vyanzo hivyo kinyume
cha sheria na kuchochea machafuko katika maeneo hayo.
Waziri wa Ulinzi wa
Uganda ameongeza kuwa, kukosekana usimamizi mzuri wa vyanzo hivyo, kunaweza
kuwa moja ya njia zinazochochea kuzuka makundi ya kigaidi katika maeneo hayo.
Aidha viongozi hao wamejadiliana suala la kutiwa mbaroni Jamil Mukulu, kiongozi
wa kundi la waasi wa ADF ambao wanatuhumiwa kufanya mauaji ya karibu watu 300
tangu mwezi Oktoba mwaka jana huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo. Kiyonga amesema kuwa, Mukulu atakabidhiwa kwa serikali ya Uganda
karibuni hivi.
0 comments:
Post a Comment