Baada ya Liberia kutangaza kumalizika kwa
maambukizi ya Ebola tarehe 9 Mei, idadi ya wagonjwa wa Ebola nchini Sierra
Leona na Guinea imekuwa ikipanda na kushuka, ambapo wiki iliyopita, WHO
iliripoti wagonjwa wapya 12 wa Ebola, 9 kutoka Guinea, na 3 Sierra Leone. Bw.
Aylward amesema, kama kazi zitaendelea vilivyo, Sierra Leone na Guinea
zitakomesha Ebola mwezi Septemba mwaka huu, lakini kuna uwezekano maambukizi
hayo yakaendelea hadi mwishoni mwa mwaka huu.
Amesema, mbali na upungufu wa fedha, vita
dhidi ya ebola inakabiliwa na changamoto nyingine kwa mfano msimu wa mvua ambao
umeanza katika Afrika Magharibi na kuweza kuongeza maambukizi ya magonjwa kama
malaria na kuhara, hali ambayo itaongeza ugumu wa kuthibitisha kesi ya Ebola
kutokana na hali zinazofanana.
0 comments:
Post a Comment