Suala muhimu la awamu ya tatu ya Rais Pierre
Nkurunziza halikuchukuliwa uamzi katika mkutano huo au hata kujadiliwa na
marais hao wa nchi za Afrika Mashariki. Watu wamechukizwa na jambo hilo na wako
tayari kuendelea na maandamano.
Katika wilaya za mji wa Bujumbura
kunakofanyika maandamano kama Cibitoke na Nyakabiga, raia wamekata tamaa.
Lakini pia wamekua na hasira, baada ya mapendekezo yaliyotolewa katika mkutano
wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki.
Wakaazi wa wilaya hizo walikua na matumaini
kuwa viongozi hao kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki wangemtaka rais
Pierre Nkurunziza kuacha kuwania awamu ya tatu. Suala la kuahirishwa kwa
uchaguzi kwa mwezi mmoja na nusu halina mabadiliko yoyote katika msimamo wao.
" Tumekataa tamaa moja kwa moja, kwa
sababu hawakusema chochote kuhusu awamu hii ya tatu ya rais Nkurunziza. Marais
wa kanda hii hawana uwezo wa kumshawishi Nkurunziza kuacha kuwania awamu ya
tatu. Tunahitaji jumuiya ya kimataifa kutusaidia ili tuweze kukabiliana na
mgogoro huu ", amesema raia
mmoja aliyehojiwa na RFI.
" Hatukua na matumaini makubwa kuhusu
mkutano huo. Tuna machungu kutokana na uamzi huo. huo ni usaliti wa moja kwa
moja. Tutaendelea kuandamana, tutaendelea na harakati zetu. Lakini ukweli
hatimaye utashinda ", wamesema
raia wangine wa mji wa Bujumbura.
Serikali ya Burundi imekaribisha mapendekezo
ya marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kuahirisha Uchaguzi kwa angalau mwezi
mmoja na nusu ili kukabiliana na hali ya kisiasa nchini humo.
Hata hivyo upinzani unasema umesikitishwa na
mapendekezo ya marais hao waliokutana mwishoni mwa juma lililopita jijini Dar
es salaam na wameapa kuendelea na maandamano makubwa jijini Bujumbura leo
Jumatatu.
Pacifique Nininahazwe kiongozi wa maandamano
amesema kuwa wamesikitishwa kuwa viongozi hao wameshindwa kumwambia rais
Nkurunziza kutowania urais kwa muhula wa tatu.
Uchaguzi wa wabunge nchini Burundi umepangwa
kufanyika tarehe tano mwezi huu, huku ule wa urais ukifanyika tarehe 26.
Itafahamika kwamba rais wa Burundi Pierre
Nkurunziza hakushiriki mkutano huo na aliwakilishwa na waziri wake wa mambo ya
nje Alain Nyamitwe. Hata rais wa Rwanda Paul Kagame alisusia mkutano huo,
akibaini kwamba viongozi wa jumuiya ya Afrika Mashariki wamekua wakipigana
chenga kuhusu uamzi mabo unapaswa kuchukuliwa dhidi ya muhula wa tatu wa rais
Pierre Nkurunziza.
0 comments:
Post a Comment