Wananchi wa eneo hilo wamesema uhaba huo wa maji
umekuwa ukisababisha matumizi ya maji yasiyo safi na salama na kuwalalamikia
viongozi wa eneo hilo kushindwa kutatua tatizo hilo sambamba na kukosekana kwa
ushirikishwaji mzuri wa mipango ya maendeleo hali inayosababisha pia matabaka
baina ya viongozi na wananchi.
Mwenyekiti wa mtaa wa FULWE Said Katembo ameelekeza
lawama kwa watendaji wa halmashauri ya wilaya kwa kukosa ushirikiano na
viongozi wa vijiji, hivyo kushindwa kufikisha huduma zinazo tolewa na serikali
ikiwemo vocha za pembejeo kwa wakulima
pamoja na kuwepo kwa mikataba ya kughushi ya wapokeaji wa ruzuku hizo,huku mkuu
wa wilaya ya Morogoro Jordan Rugimbana aliyetembelea eneo hilo,akiahidi
kukabiliana na malalamiko hayo na kusisitiza
uzingatiwaji wa ujenzi wa maabara katika kata zote ili kupata wataalam
wenye ujuzi wa kutosha kusaidia kuleta maendeleo katika vijiji na taifa kwa
ujumla.
0 comments:
Post a Comment