Pluijm aliondoka nchini mara baada kuiongoza
timu hiyo ya Jangwani kwa msimu wa 2014/15 na kutwaa kutwaa ubingwa ikiwa
imesalia na michezo miwili mkononi.
Katibu Mkuu wa kikosi hicho, Dk. Jonas
Tiboroha alisema kuwa pindi kocha huyo atakapowasili, timu hiyo itaanza mazoezi
rasmi kwa ajili ya kuanza maadalizi ya msimu ujao.
Tiboroha aliyekuwa akihojiwa na kituo kimoja
cha redio alisema wachezaji wa wapya na wale wa wanaondelea na mkataba yao
wataanza kuwasili klabuni hapo kuanzia leo.
Tofauti na hilo, Dk. Tiboroha alisema kuwa
katika mazoezi hayo yatakayoanza muda mfupi baada kocha kuwasili kutakuwepo na
wachezaji kadhaa wa kigeni ambao watakuwa katika
mchujo.
mchujo.
“Katika kambi hiyo kutakuwepo na wachezaji
kadha wa kigeni ambao nao wataungana na wachezaji wengine kwa ajili ya kufanya
mazoezi ya pamoja ili kutafuta nafasi ya kusajiliwa kwa ajili msimu ujao na
atakayefuzu tunaweza kuwa naye,” alisema.
Hata hivyo alisema katika usajili wa
wachezaji wa kigeni utasubiri kupata ridhaa ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kwa maana hadi sasa tayari kikosi hicho kina wachezaji watano.
Yanga ni miongoni timu zinazotaka TFF
kurekebisha sheria za kusajili wachezaji wa kigeni kwa kuongeza idadi ya watano
hadi wanane ili kutoa fursa ya kukiimalisha kikosi chao.
Wachezaji watano wa kigeni ambao
wanaokitumikia kikosi hicho ni Andrey Coutinho (Mbrazil), Mbuyu Twite na Haruna
Niyonzima (Rwanda), Kpah Sherman (Liberia), Amissi Tambwe.
Baadhi ya wachezaji wa kitanzania ambayo
tayari wameshatua katika kikosi hicho ni Deus Kaseke na Malimi Busungu
wanandinga ambao wanaaminika watakuwa chachu ya ushindi na kuchukua ubingwa
msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment