Mbali na hilo, wapinzani wameonya makada wa
chama hicho wanaotangaza nia ya kuwania urais kuacha kutumia sera hiyo ya
upinzani kwa sababu walikuwa Serikalini tangu uhuru na wameshindwa kufanya
hivyo.
Akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo bungeni
jana kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Msemaji Mkuu kwa kambi hiyo katika Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo, alisema elimu haijawahi kuwa
kipaumbele katika sera za CCM kwa awamu zote za utawala wake na ndiyo maana
imeshindwa kutekeleza hata Ilani yake ya uchaguzi.
“Sera ambayo CCM imepigia upatu kwa miaka
yote 53 ya uhuru na ambayo pia imeshindwa kutekeleza ni kilimo, ndiyo maana
tangu enzi za uongozi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere sera
zilizosikika ni Siasa ni Kilimo, Kilimo cha Kufa na Kupona, Kilimo ni Uti wa
Mgongo wa Taifa na sasa Kilimo Kwanza. Hatujawahi kusikia elimu kwanza kwa
utawala wa CCM kwa miaka yote 53 ya Uhuru,” alisema.
Suzan ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu
(Chadema) alisema sera ya elimu kwanza ni ya upinzani na kwamba ipo katika
ilani ya uchaguzi ya Chadema ya mwaka 2005 na 2010 na imepewa kipaumbele cha
kwanza, cha pili na cha tatu.
“Itakumbukwa kwamba Chadema iliposema elimu
bure kama ingechaguliwa kuunda serikali mwaka 2005 na 2010, CCM iliendesha
propaganda chafu ya kuwapotosha wananchi kwamba haiwezekani kutoa elimu bure.
“Lakini ili kuthibitisha ile methali isamayo
kwamba njia ya muongo ni fupi, CCM hivi sasa imekubali kula matapishi yake na
kusema katika kipengele cha 3.1.5 cha sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 kwamba
elimu itakuwa bure,” alisema na kuongeza:
“Huu ni uthibitisho kuwa CCM imebobea katika
wizi hadi kufikia hatua ya kuiba sera ya upinzani waziwazi bila aibu. Ukawa
ikitwaa madaraka ya dola katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, elimu ya msingi
hadi Chuo Kikuu itakuwa bure.”
Sera mpya ya elimu
Kuhusu sera mpya ya elimu, alisema imekuwa
hazitekelezeki kwa kuwa ni sera bainishi na imekuwa ikibainisha upungufu pekee
na kuacha sehemu ya utekezaji.
Alisema ili sera hiyo iweze kutekelezeka ni lazima kuwapo na walimu bora, zana bora za kufundishia na walimu wenye motisha.
Alisema ili sera hiyo iweze kutekelezeka ni lazima kuwapo na walimu bora, zana bora za kufundishia na walimu wenye motisha.
“Tanzania imekuwa ikisifika kwa kuandika
vizuri sera zake, lakini utekelezaji wake ni shida. Mfano sera hii haielezi ni
kwa kiasi gani itaondoa ubaguzi au matabaka ya elimu hasa viwango vya elimu.
Pia haielezi nini maana ya kufuta ada ikiwa kuna michango mingi kuliko ada
yenyewe,” alisema.
Dk. Kawambwa
Awali akiwasilisha hotuba yake, Waziri wa
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema kwa kushirikiana na
Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mikakati ya Matokeo
Makubwa Sasa (BRN) imetekelezwa.
Alisema sekta ya elimu imefanikiwa kwa
asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza
ya mikakati hiyo.
Dk. Kawambwa aliainisha vipaumbele vya sekta
ya elimu vilivyomo katika mwongozo wa taifa wa maandalizi ya mpango wa bajeti
kwa mwaka 2015/2016 kuwa ni
pamoja na kuongeza upatikanaji wa fursa ya elimu kwa usawa katika ngazi zote za elimu na mafunzo, kuinua ubora wa elimu na kujenga stadi stahiki, kuimarisha taasisi za usimamizi wa ubora wa elimu na ufuatiliaji na tathmini ili zitekeleze majukumu yake.
pamoja na kuongeza upatikanaji wa fursa ya elimu kwa usawa katika ngazi zote za elimu na mafunzo, kuinua ubora wa elimu na kujenga stadi stahiki, kuimarisha taasisi za usimamizi wa ubora wa elimu na ufuatiliaji na tathmini ili zitekeleze majukumu yake.
0 comments:
Post a Comment