Waziri wa nchi,ofisi ya rais kazi
maalum,Prof.Mark Mwandosya ametangaza nia yake ya kuomba kuteuliwa na chama cha
mapinduzi kugombea nafasi ya rais kwenye uchaguzi mkuu ujao,huku akisema kuwa
endapo atapata ridhaa hiyo, kipaumbele chake kitakuwa ni kujenga uchumi imara
wa taifa na watanzania kwa ujumla.
Prof.mwandosya,amesimama mbele ya umati mkubwa
wa wakazi wa jiji la mbeya na kutangaza rasmi nia yake ya kutaka kukiomba chama
chake,chama cha mapinduzi kumteua kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais kwenye
uchaguzi mkuu ujao.
Kabla ya Prof. Mwandosya kutangaza nia yake,
baadhi ya viongozi wa dini,viongozi wa mila na wanasiasa wakapewa nafasi ya
kuzungumza, ambapo wengi wao wamedai kuwa Prof. Mwandosya amelitumikia taifa
kwa muda mrefu bila kuwa na kashfa ya aina yoyote,hivyo anastahili kuliongoza
taifa la Tanzania.
Prof.Mark Mwandosya ambaye pia ni mbunge wa jimbo
la rungwe mashariki,kupitia hadhira hiyo akatangaza kuwa endapo watanzania
watampa ridhaa ya kuwaongoza kama rais,kipaumbele chake kitakuwa ni kujenga
uchumi imara wa taifa na watanzania kwa ujumla.
Prof. Mwandosya ametangaza kwenda kuchukua fomu
dodoma siku ya jumatano wiki hii ambapo zaidi ya shilingi milioni 10
zilichangwa na wananchi kwa ajili ya kumuwezesha kuchukua fomu hiyo.
0 comments:
Post a Comment