Timu hizo kila zinapochuana zimekuwa
zikionyesha upinzani mkubwa, hasa kutokana na uhasama mkubwa waliokuwa nao kama
zilivyo timu za Simba na Yanga kwa Tanzania.
Ulimwengu ‘Rambo’ aliyekuwa kwenye kiwango
bora, alifanya mauaji hayo katika mashindano maalumu ya urafiki yaliyomalizika
juzi, mabao mengine ya Mazembe yalifungwa na Cheibane Traore na Adama Traore,
huku Clovis Mbayi akiifungia Lupopo bao la kufutia machozi.
TP Mazembe, iliyoukosa ubingwa wa Ligi Kuu
Kongo msimu huu uliochukuliwa na AS Vita, imemaliza vema michuano hiyo kwa
mafanikio na kufuta machungu ya kushika nafasi ya pili kwenye ligi.
Ulimwengu na Mtanzania mwingine, Mbwana
Samatta, wanaokipiga kwa matajiri hao wa jiji la Lubumbashi, wameitwa na Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, Mart Nooij, kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo wa kufuzu Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017 dhidi ya Misri,
utakaofanyika Juni 14, jijini Alexandria, Misri.
Mbali na kucheza na Misri, Stars, iliyopangwa
Kundi G, itacheza na kigogo kingine cha Afrika, Nigeria pamoja na Chad, ambao
wanaonekana kama vibonde.
0 comments:
Post a Comment