Cassilas amekuwa majeruhi kwa muda mrefu
baada ya kuumia goti walipokuwa kambini nchini Afrika Kusini mwaka jana, hali
iliyopelekea kukaa muda mrefu bila kucheza, ambapo inadaiwa uongozi wake
unataka kumtoa kwa mkopo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Cassilas
alisema yupo tayari kuondoka Simba, lakini si kwa kutolewa kwa mkopo na
kusisitiza kuwa anajiamini kutokana na uwezo mkubwa wa kudaka aliokuwa nao.
“Najiamini na kazi yangu ndiyo maana mpaka
sasa timu yangu inanihitaji kutokana na kazi yangu ninayoifanya, isitoshe,
nimeshakuwa kipa bora kwa misimu miwili mfululizo, kwa hilo najivunia,”
alisema.
Alisema atakaporudi kazini ataendelea kufanya
vizuri zaidi, hivyo mashabiki wategemee mambo mazuri zaidi atakaporudi dimbani
rasmi kutokana na kumkosa kwa muda mrefu alipokuwa majeruhi.
Kamati ya Usajili ya Simba chini ya
Mwenyekiti, Zacharia Hans Poppe, wameiongezea nguvu safu ya langoni baada ya
kuonekana kulegalega msimu uliopita na kupelekea Simba kushika nafasi ya tatu.
Mpaka sasa imemsajili kipa mpya kutoka JKU ya
Zanzibar, Mohamed Abraham Mohamed, aliyefanya safu hiyo kuwa na makipa watano,
wengine wakiwa ni mkongwe, Ivo Mapunda, Manyika Peter Jr, Casillas pamoja
na kipa aliyepandishwa kutoka timu ya vijana, Denis Richard.
Hivyo, kuna hofu kubwa ya Casilas na Richard
kuenguliwa kwenye usajili wa timu hiyo kwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL).
0 comments:
Post a Comment