Uyoga ni moja ya mboga ambayo imekuwa ikiliwa na baadhi ya watu hapa
nchini, lakini je, umewahi kuwaza kuwa mboga hiyo inaweza kuwa dawa? Na
kama dawa unadhani ni dawa ya nini hasa?
Majibu ya maswali hayo yanapatikana kutoka katika hii stori kutoka
nchini Taiwan, ambapo wao uyoga kwao hutumika kama dawa ya kupunguza
unene.
Kwa miaka sasa uyoga umekuwa ukitumika nchini humo kama dawa ya
kupunguza unene katika wanyama, hayo yamesemwa na watafiti nchini
Taiwan.
Utafiti huo, uliochapishwa katika jarida la mawasiliano ya mazingira umebainisha kuwa madini ya 'Ganoderma Lucidum' yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kuwa na uzito mkubwa kwa kutatiza bakteria ndani ya utumbo.
Imeelezwa kuwa madini hayo ya 'Ganoderma Lucidum' yaliyomo ndani ya uyoga, hupunguza taratibu uwezo wa mtu kupata uzani
Wataalam wanasema kuwa sayansi hiyo ni nzuri, lakini kuweka maji
yanayotokana na uyoga kwenye mikebe ya cola hakutawasaidia watu
kupunguza uzani.
Mbali na hayo Watafiti katika chuo Kikuu cha Chang Gung wamesema kuwa
madini hayo ya G. lucidum yameuwa yakiuzwa tangu jadi kama kichocheo cha
"kiafya na kurefusha maisha"
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment