Akihutubia katika mkutano wa kuhitimisha ziara
yake, jijini Mwanza jana, Kinana alisema atafanya kikao cha kwanza na
wabunge wa CCM baada ya uchaguzi ili kuwaeleza majukumu yao ya msingi
ikiwamo kuiwajibisha Serikali.
Alisema wabunge wa CCM wamekuwa wakiunga mkono
kila jambo linaloletwa bungeni bila kutathmini matokeo ya sheria hizo
kwa wananchi wanaowawakilisha.
Alisema lazima ifike wakati wabunge wa CCM wabadilike na kuwatumikia wananchi wao.
“Nitakutana na wabunge wa CCM na kuwaambia kwamba
sheria walizozipitisha haziwasaidii wananchi… lazima chama kiwe na nguvu
ya kuielekeza au kuiwajibisha Serikali yake,” alisema Kinana huku
akishangiliwa na wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Katibu Mkuu huyo alisema kuna haja ya kubadilisha
mfumo wa utendaji kazi wa chama na mojawapo ni kuchagua mtu mwingine wa
kuongoza wabunge wa CCM bungeni badala ya Waziri Mkuu kama ilivyo sasa.
Alisema Waziri Mkuu ataachwa atekeleze jukumu lake
la kuiongoza Serikali bungeni, lakini kuwe pia na kiongozi wa wabunge
wa CCM bungeni. Alisema mfumo huo utakipa chama nguvu zaidi ya
kuisimamia Serikali yake.
“Wamekaa wabunge tena na kupitisha sheria ya kila
gari kuwa na kizimamoto, nani alisema gari langu lina mpango wa
kuungua?” alihoji kiongozi huku na kusema sheria nyingine zinatakiwa
kufutwa kwa sababu hazimsaidii mwananchi.
Aliishangaa Serikali ya CCM kwa kushindwa kufuta
baadhi ya sheria ambazo zimebainika kuleta usumbufu kwa wananchi na
kusisitiza kuwa lazima ifike wakati Serikali ifanye tathmini ya sheria
zake na kuzifuta ambazo hazifai kwa sasa.
“Nimekuwa waziri na kiongozi serikalini kwa muda
mrefu, lakini sijawahi kuona Serikali ikifuta sheria. Wamekuwa
wakiongeza sheria mpya kila siku. Hivi karibuni Serikali imepeleka
miswada mingine 11 na yote imepitishwa. Kwa namna hiyo tunambebesha
mwananchi mzigo mkubwa,” alisema.
Kinana aliitaka Serikali kuwashirikisha wananchi
wakati wa kutunga sheria ili kuondoa changamoto ambazo zimekuwa
zikijitokeza mara kwa mara.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwapigia saluti, maelfu ya wananchi, alipowasili kuhutubia mkutano wake wa hadhara aliofanya leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza.Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiwahamasisha maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika leo katika Vianja vya Furahisha Jijini Mwanza.
"'SAFI SANA"Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana aonyesha dole gumba ambayo ni ishara ya CCM na kuonyesha kuwa mambo safi, alipowasili kuhutubia mkutano wa hadhara leo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye.
Malikia wa taarab, Khadija Kopa akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM, wakati wa mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrhmn Kinana uliofanyika leo, kwenye Uwanja wa Furahiha jijini Mwanza |
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wake wa hadhara aliofanya katika Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
Maelfu wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipohutubia mkutano wa hadhara katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
Maelfu wakiwa wamefurika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika Viwanja hivyo leo.
Aliyekuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi y Chadema, katika uchaguzi mkuu uliopita, Twalib Ngika, akikabidhi yadi ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinna baada ya kutangaza kuhamia CCM, wakati wa mkutano wa hadhara wa Katibu Mkuu huyo uliofanyika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza leo
Kinana akisindikizwa na maelfu ya wananchi alipokuwa akiingia kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika leo. Pmoja naye ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Anthony Diallo n Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo.
Wananchi wakishangilia kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, Anthony Diallo, akihutubia mkutano huo.
Mmoja wa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano huo, akiwa na mtoto wake aliyeshika kipeperushi cha CCM. |
Meya wa Jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula akihutubia kwenye mkutano huo.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia kwenye mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihitimisha kwa hotuba katika mkutano wake wa hadhara uliofanyika katika Viwanja vya Furahisha jijini wanza leo.
0 comments:
Post a Comment