Vikosi
vya Usalama nchini Chad vimewatia mbaroni watu 60 wanaotuhumiwa kuwa ni
wanamgambo waliohusika na mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga
kwenye Mji mkuu wa Chad, N'Djamena tarehe 15 mwezi huu.
Milipuko
miwili ya mabomu ya kujitoa muhanga kwenye ofisi
mbili za Polisi Mjini N'Djamena, ambayo inaonekana kuratibiwa na
wapiganaji wanne wa kikundi cha Kiislam cha Boko Haram na kusababisha vifo
vyawatu 34 wakiwemo watuhumiwa wanne wa
Boko Haram na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Mwendesha
Mashitaka mkuu nchini Chad, Bwana
ALGHASSIM KHAMIS amesema katika operesheni hiyo mtandao wa ugaidi wa
Boko Haram umeteketezwa.
Amesema
wapiganaji wa Boko Haram waliotiwa mbaroni wanatoka mataifa ya Chad, Cameroon,
Mali na Nigeria.
0 comments:
Post a Comment