Wanajeshi 11 wa Afghanistan wameuawa katika shambulio
la kushitukiza lililofanywa na wapiganaji wa Taliban, Magharibi mwa nchi hiyo.
Msemaji
wa gavana wa Jimbo la Herat, Bwana
EHSANULLAH HAYAT, amesema
wapiganaji hao wa Taliban waliushambulia msafara wa wanajeshi hao
katika Wilaya ya Karukh jana usiku na
kusababisha vidfo vya wanajeshi hao 11.
Amesema
wanajeshi hao walikuwa wakisafiri kwenye magari madogo ya mizigo Pick-Up.
Naye
Msemaji wa Jeshi Magharibi mwa
Afghanistan Bwana NAJIBULLAH NAJIBI, amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo
na kuongeza wanajeshi wanne pia wamejeruhiwa katika tukio hilo.
Wanajeshi
wa Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi
- NATO- wakiongozwa na Marekani waliondoka Afghanistan Desemba mwaka
jana na kuwaacha maafisa wachache kwa ajili ya kutoa mafunzo na kuvisaidia
vikosi vya usalama.
0 comments:
Post a Comment