Karibu leo tuvifahamu hivi vyakula na matunda ambavyo ni muhimu kwa siha ya ngozi zetu.
Sehemu kubwa ya miili yetu ni ngozi na ni sehemu muhimu ya mwili ambayo
ina jukumu kubwa la kuukinga mwili dhidi ya matatizo mbalimbali, hivyo
afya ya ngozi ni vizuri ikazingatiwa.
Vyakula tunavyokula vinaweza kuchangia katika kutengeneza muonekano
mzuri wa ngozi yako na kusaidia kupambana na matatizo ya ngozi.
Kimsingi ni kweli kwamba kila mtu hupenda kuonekana vizuri, lakini
huenda ukashindwa kufikia lengo hili la kuonekana vizuri kwasababu ya
kutofahamu njia sahihi ya kudumisha afya za ngozi yako.
Wataalam wa lishe wanasema kwamba kila tunachokula huwa ni moja ya
sehemu ya miili yetu ikiwa ni pamoja na sehemu ya nje, hii inamaana kuwa
kila tunavyokula vyakula bora ndivyo ngozi zinavyoonekana vizuri zaidi.
Vifuatavyo ni vyakula vinavyoweza kusaidia kuimarisha afya ya ngozi:-
Asali ambayo hutengenezwa na nyuki huwa na viambato asilia na ni moja ya
chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi . Asali husaidia
kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha
sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi.
Tumia asali kwa kupaka wakati wa kuoga, kisha acha kwa muda na ioshe. Kufanya hivyo husaidia kuinawirisha ngozi.
Mayai pia ni muhimu kwa afya ya ngozi yako, kiini cha yai huwa na
vitamini A na B, huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo
ni muhimu pia kwa ngozi, ute wa yai ni muhimu katika kuifanya ngozi kuwa
nyororo na yenye kung'aa na pia husaidia ngozi kujilinda vizuri na
mionzi ya jua.
Matunda nayo ni muhimu pia hususani chungwa na limao ambayo husaidia
kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen,
ambayo ni aina ya protini inayotengeneza ngozi.
Ndani ya matunda hayo huwa na Vitamini C , ambayo husaidia sana kuondoa
uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.
Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama tujuavyo
zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida
kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla. Mboga hizi za majani kwani husaidia
ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza
ukavu na kutunza ngozi na kuifanya ing’are na kuvutia.
Vyakula vya baharini kwa ujumla ni vizuri kwa afya ya ngozi. Vyakula
vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni
muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa
kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi
na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi.
Anza kupenda kula vyakula vyenye lishe bora kwa kuwa na ngozi bora zaidi.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment