Image
Image

Wao wakiitazama Ikulu, sisi tulitazame taifa huku tukiweka uchama pembeni.



                                Hamphrey polepole.
Mjadala huu, licha ya kwamba ni mzuri hasa katika jamii ya kiraia, huenda usiwe na tija sasa kwa wananchi. Ushauri wangu kwa wananchi wenzangu ni kuanza kutazama hali halisi ya nchi yetu, tumetoka wapi, tuko wapi na tunataka kwenda wapi?
Kwa hali ilivyo sasa ninaona jotoridi ikizidi kupanda katika vyama vya siasa, hasa ukizingatia michakato ya ndani ya vyama ya kuteua watakaopewa dhamana ya kugombea nafasi za udiwani, ubunge na Urais. 
Kwa kiasi kikubwa kabisa, naona Wananchi wakigubikwa na mjadala wa nani ni nani na huenda nani atapata nini. 
Mjadala huu, licha ya kwamba ni mzuri hasa katika jamii ya kiraia, huenda usiwe na tija sasa kwa wananchi. Ushauri wangu kwa wananchi wenzangu ni kuanza kutazama hali halisi ya nchi yetu, tumetoka wapi, tuko wapi na tunataka kwenda wapi?

Tukijua tumetoka wapi, tuko wapi na tunataka kwenda wapi,itakuwa rahisi kujua haiba na wajihi wa mtu ambaye tunamtaka kwa nafasi ya udiwani, ubunge na urais na hatutajikita katika kujadili watu na kujifunga na ushabiki wa kambi moja dhidi ya nyingine au chama kimoja dhidi ya kingine.

Ifike mahala mjadala wetu kuelekea uchaguzi, ili uwe na tija, tuutazame kwa msingi kwamba, licha ya nchi yetu kuwa na changamoto nyingi, tuna matarajio fulani kama raia, tuna ndoto za nchi na Taifa tunalolitaka. 
Tukitazama amani katika Taifa letu, amani ya mtu mmoja mmoja, amani katika jamii zetu, usalama wetu, tukilitazama hili tuko wapi na tunataka kwenda wapi. 
Tukiutazama umoja wa Taifa letu, tumekuwa tukijinasibu na kauli kama “umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu”. Je tukiutazama kwa jicho la karibu umoja wa Taifa letu ukoje? 
Umoja kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar, lakini hata Zanzibar, tutazame umoja kati ya Unguja na Pemba, tuangalie umoja katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa inayomaliza muda wake hivi karibuni.

Huku Bara tutazame umoja kati ya dini mbalimbali, lakini pia tutazame umoja wetu kisiasa. Tuna Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na Baraza la Vyama vya Siasa, niwaulize tija ya kuwa na taasisi hizi muhimu katika kujenga mustakabali wa siasa zetu sasa na baadaye iko wapi? Juzi tu hapa mchakato wa Katiba umekwamishwa kwa makusudi na sikuona umoja wa kisiasa wa vyama vyote au wanasiasa wote wenye mapenzi mema waliosimamia kweli ili kuokoa mchakato huu wa kihistoria.

Nimeangazia amani na umoja wa Taifa, nikijua misingi ya uwepo wake ni haki na usawa, je haki za watu na raia wa Taifa letu zinalindwa, zinatunzwa, zinahifadhiwa na kutolewa kikamilifu? Bila unafiki na kwa jibu lolote lile unaloona jema, je, haki hizi zinapatikana kwa usawa? Usawa kati ya wasio nacho na walio nacho, usawa kati ya masikini na matajiri, usawa kati ya wakulima, wafanyakazi na wafanyabiashara wadogo, usawa kati ya maeneo ya mijini na maeneo ya pembezoni?

Tunaweza tukajadili usawa wa haki, lakini pia usawa wa fursa, hivi ni nani katika Taifa letu ambao wananufaika na mikopo ya mabenki? Hivi ni nani katika Taifa letu ambao wananufaika kwa haraka na fursa za ajira? Utasema labda tuangalie tu miongoni mwa vijana upatikanaji wa fursa za ajira ukoje? Lakini juzi hapa natazama taarifa ya habari nikasikia katika jiji la Mwanza kuna ongezeko kubwa la wazee wasio na ajira. Hii tafsiri yake nini? Tunatoka wapi, tuko wapi na tunataka kuelekea wapi? Tukijikita katika mjadala huu na kulitazama Taifa hatutakuwa na muda wa kuzongwa na mbwembwe za watangazania ambao nia yao- na nikiwasikiliza wengi- ni kufika Ikulu wakati sisi tunataka tufike kule katika nchi ya ahadi ambayo wananchi, watu na raia wa Taifa letu wanastahili kuwepo.

Kiongozi anayeweza kusimamia amani na umoja unaojengwa katika misingi ya haki na usawa, ni yule mwenye uthubutu, ni yule asiyeona haya kusimama na Watanzania, mwenye hekima, mpole, baba wa wote, ambaye ni ishara ya umoja wetu, ambaye jamii inamuamini na sisi tunajua kwa hakika anajua matatizo yetu na tukimuona tunajua ana dhamira ya kweli kutufikisha katika Tanzania tunayoitaka, kwanza kwa kuijengea misingi imara na pili kutuleta kama Taifa pamoja.

Elimu ya kuhamasisha uandikishaji

Nina uhakika kwamba kila Mtanzania mwenye sifa ya kupiga kura amejiandikisha, ama yuko anajiandikisha au ameshajiandaa tayari kuandikishwa wakati Tume ya Taifa ya Uchaguzi itakapofika eneo lake. Na kwa wale ambao kwa namna moja au nyingine, kwa makusudi au kwa bahati mbaya wameikosa haki yao ya kikatiba ya kuandikishwa kwenye daftari la wapiga kura, naomba mjitokeze mara moja sasa ili Tume ya Uchaguzi itimize ile ahadi yake kwamba hakuna raia mwenye sifa ya kuandikishwa atakayeachwa kuandikishwa.

Nitoe rai kwa wananchi wenzangu hasa wale wenye sifa ya kuandikishwa na hawajaandikishwa bado wajitokeze, ili sote tusaidie kuikumbusha Tume ili iwaandikishe wakati muda ungalipo.

Pia nimefuatilia hoja za wanafunzi vyuoni majibu ya Tume ya Uchaguzi. Wanafunzi wana hofu juu ya maeneo wanapoandikishwa au watakapojiandikisha na uhalisia wa eneo watakalopigia kura Oktoba 25, hapa kuna hoja. Kama zoezi linavyoendelea kutoka mwanzoni mwa mwaka huu ni hakika kuna wanafunzi wengi watakuwa wameandikishwa wakiwa mashuleni na vyuoni kwao na wakati wa kupiga kura ama watakuwa shuleni na vyuoni au watakuwa likizo.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, kutakuwa na fursa ya kubadili eneo la kupigia kura, ambayo mpigakura kule ambako anajua atakuwa mwezi Oktoba basi atakwenda na kuboresha taarifa zake na hapo ndipo Tume itahamisha taarifa zake za ukaazi wa awali kwenda eneo jipya atakalopigia kura. Fursa hii ya kubadili taarifa za ukaazi kutoka eneo moja kwenda jingine itakuwapo kati ya Agosti 11 na 18. Rai yangu kwa wanafunzi wote ni kuzingatia fursa hii.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment