Tangazo la kuondolewa kwa muswada huo lilitolewa juzi bungeni na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya aliyesema
uamuzi huo unalenga kuufanya uboreshwe na kupunguza madhara yanayoweza
kutokea kwa jamii baadaye.
Juzi Serikali ilikubali kuundoa Muswada wa Sheria ya Upatikanaji Habari ya 2015 ili upelekwe kwa wadau kwa lengo la kuujadili na kukubaliana katika vipengele ambavyo wameviona vina matatizo.
Juzi Serikali ilikubali kuundoa Muswada wa Sheria ya Upatikanaji Habari ya 2015 ili upelekwe kwa wadau kwa lengo la kuujadili na kukubaliana katika vipengele ambavyo wameviona vina matatizo.
Tangazo la kuondolewa kwa muswada huo lilitolewa
juzi bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa
Mark Mwandosya aliyesema uamuzi huo unalenga kuufanya uboreshwe na
kupunguza madhara yanayoweza kutokea kwa jamii baadaye.
Muswada huo, ambao ulikuwa unapingwa vikali na
wanahabari na wadau, wakiongozwa na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya
Habari (MOAT), Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri (TEF),
ulichapishwa Februari 20, 2015 na kusomwa kwa mara ya kwanza kwenye
vikao vya Bunge vya Machi hadi Aprili.
Ulitakiwa usomwe kwenye Bunge la Bajeti
linaloendelea mjini Dodoma, lakini wanahabari waliongeza sauti ya kilio
chao na kusababisha Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii kujadili kwa
kina na kufikia uamuzi.
Akisoma taarifa ya Serikali, Profesa Mwandosya
alisema baada ya kupokea maoni ya Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii,
Serikali imetafakari na kuafiki kuwa muswada huo uendelee kufanyiwa kazi
hadi hapo kazi hiyo itakapokuwa imekamilika ipasavyo.
Alisema matarajio ya Serikali ni kwamba muswada
huo utasomwa kwa mara ya pili na ya tatu kwenye Bunge la Kumi na Moja
ambalo litapatikana baada ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Oktoba
25 mwaka huu.
Hizi ni habari njema kwa waandishi wa habari na
wadau wote wa tasnia ya habari kwamba hatimaye Serikali imesikia kilio
chao na kuamua hatua zinazotakiwa za kuupitisha muswada huo katika hatua
mbalimbali, zifanyike ili baadaye muswada uende bungeni ukiwa na ridhaa
ya pande zote.
Tunapenda kuipongeza Serikali kwa uamuzi huo wa
busara wa kusikiliza kilio cha wanahabari, ambao hadi sasa wanafanya
kazi kwenye mazingira magumu kutokana na kuwapo kwa sheria za kibabe
ambazo nyakati fulani hutumiwa vibaya na kuwaumiza.
Huu ndiyo ungekuwa motto wa utendaji kazi wa
Serikali wa kuhakikisha inashirikisha wadau katika masuala muhimu
yanayowahusu watu wa sekta husika kabla ya kufanya uamuzi.
Dhana ya ushirikishwaji ndiyo inayotawala katika
ulimwengu wa kisasa ambao umejaa watu waliosoma, waliopevuka, weledi na
wenye uwezo wa kuchambua mambo. Katika dunia ya namna hiyo ni vigumu
kuwaburuza watu katika kufanya uamuzi kwa kuwa utakabiliwa na upinzani
mkubwa.
Hali kadhalika, dhana ya ushirikishwaji inaandaa
mazingira ya kuiwezesha sheria inayoundwa kutekelezeka kwa kuwa inakuwa
imepata ridhaa ya pande zote ambazo zinakuwa zimeshiriki kikamilifu
tangu hatua za awali hadi mwisho.
Tunapenda kuipongeza Serikali kwa uamuzi huo na
tunaamini kuwa itaendelea kusikiliza wadau wa sekta mbalimbali kila
inapotaka kufanya uamuzi ambazo unawagusa wahusika.
0 comments:
Post a Comment