Image
Image

Wadau wahoji uwezo wa Mvella TFF.


BAADHI ya wadau wa soka nchini wamehoji vigezo ambavyo vimetumika hadi sasa Kaimu Mkurugenzi wa Vyama na Masuala ya Sheria wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Eliud Mvella kuendelea kushikilia nafasi hiyo ilhali vigezo hana.
Wasiwasi huo umekuja baada ya kuona hadi sasa TFF wapo kimya kutafuta mbadala wa Evodieus Mtawala, ambapo kisheria Mvella alitakiwa kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi sita, lakini imepita na hakuna chochote kinachoendelea.
Sheria zinasema endapo miezi sita ya kukaimu ikipita, inatakiwa athibitishwe mtu mwingine au yule aliyekaimu kama anavigezo vifuatavyo; awe mwanasheria pia na cheti ya uwakili  ngazi ya juu.
Awali nafasi hiyo ilikuwa ikishikiliwa na Wakili Evodius Mtawala ambaye alibwaga manyanga kwa madai kuwa ukiritimba uliokithiri ndani ya shirikisho hilo  pamoja na miundombinu mibovu ya utendaji ndani ya TFF ndio chanzo cha mwanasheria huyo kuamua kujiweka pembeni.
Wakizungumza na gazeti hili jana baadhi ya wadau hao, walisema kwamba ni aibu nafasi nyeti kama hiyo kushikiliwa na mtu ambaye hana uzoefu, kitu ambacho kitazidi kudidimiza soka la Tanzania.
"Kuna masuala ambayo Mvella atatakiwa kuamua lakini hana vigezo vya kushika nafasi hiyo hivyo ni vigumu kutoa maamuzi sahihi," alisema mmoja wa wadau hao ambaye yupo karibu sana na shirikisho hilo.
Katika hatua nyingine baadhi ya wajumbe wa TFF wamepanga kulifikisha suala hilo katika Kikao cha Kamati ya Utendaji kitakachokaa kesho visiwani Zanzibar.
Anayetakiwa kukalia kiti hicho cha  Ukurugenzi wa Vyama na Masuala ya Sheria anatakiwa kuwa na uzoefu ambao utasaidia sana kukabili changamoto mbalimbali za vyama wanachama wa TFF.
Pia ujuzi wa masuala ya sheria utasaidia kutatua masuala mbalimbali ya kisheria na kikatiba ndani ya shirikisho hilo, lakini kwa Mvella haipo hivyo na hivyo kujikuta watu wengine ndani ya TFF kuwa na majukumu mengi ambapo hulazimika kufanya kazi za Mvella.
Mvella alikaimu nafasi hiyo tangu Mei 21, mwaka jana, hivyo hadi sasa anazaidi ya mwaka ambapo ni kinyume na kanuni za TFF.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment