Image
Image

Rais Jakaya Kikwete kulihutubia Bunge Julai 9.


Rais Jakaya Kikwete atalihutubia Bunge la 10 mjini Dodoma kati ya Julai 9 au 10 kulingana na ratiba yake. Bunge hili litakuwa la mwisho kwa Awamu ya Nne ya uongozi wake kabla ya kuvunjwa rasmi katika tarehe itakayopangwa.
Mkurugenzi wa Idara ya Elimu kwa Umma na Ushirikiano wa Kimataifa ya Bunge, Jossey Mwakasyuka alisema hayo mjini Dodoma.
Mwakasyuka alisema sasa Bunge linaendelea na maandalizi ya ujio wa Rais Kikwete. “Rais atalihutubia Bunge kulingana na ratiba yake, lakini sisi tumeanza maandalizi ya shughuli hiyo,” alisema Mwakasyuka.
Kwa mujibu wa Kanuni za Bunge Ibara ya 30 (i), Rais anaweza kuhutubia siku yoyote wakati Bunge linapokutana.
Hata hivyo, alisema Rais hatovunja Bunge kwa sababu litavunjwa kwa Tangazo la Serikali (GN). “Imekuwa ni utamaduni Rais anapomaliza kipindi chake cha uongozi anakuja kulihutubia Bunge, pengine safari hii anakuja kueleza mambo yaliyofanywa na Serikali yake,” alisema.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, Jenista Mhagama alisema: “Suala hilo liko ofisi ya spika na kamati yake ya uongozi ndiyo watakuwa na ratiba yote.”
Alipotafutwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilila kuzungumzia zaidi suala hilo hakupatikana.
Pia kama ilivyokuwa kwa Bunge la tisa, wabunge watatunukiwa vyeti kutambua utumishi wao walioutumikia katika Bunge la 10.
Rais alilihutubia Bunge hilo la 10 kwa mara ya kwanza Novemba 18, 2010 ikiwa ni mwezi mmoja baada ya kuapishwa kushika madaraka hayo kwa kipindi cha pili.
Bunge la 9 na 10 lilipata mitikisiko mbalimbali hali iliyosababisha Rais kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment