Image
Image

Azam FC yasaka saini ya Mzambia.


Matajiri wa Chamazi, Azam wameanza harakati za kuisaka saini ya mshambuliaji wa Power Dynamos ya Zambia, Jimmy Ndhlovu anayetajiwa kutua nchini Jumatano. Makamu mwenyekiti wa Azam, Nassoro Idrissa aliliambia gazeti hili kuwa wanasaka mshambuliaji na kipa na wanategemea kufanya mazungumzo na wachezaji wanne tofauti.
“Ndhlovu atawasili Jumatano kwa ajili ya mazungumzo na kama tufafikia makubaliano tutampa mkataba, kwa ajili ya kuitumikia klabu yetu kwa msimu ujao.
Mzambia huyo katika msimu uliopita aliifungia Power Dynamos mabao 13 na timu hiyo ilimaliza kwenye nafasi ya pili.
Mbali ya Mzambia huyo, pia Azam inaendelea na jitihada zake za kuisaka saini ya mshambuliaji wa El- Merreikh ya Sudan, raia wa Mali, Mohamed Traore.
“Tunaendelea na mazungumzo na Traore, tutaangalia mmoja kati ya hao wawili.”
Pia, Idrissa alisema hivi sasa pia wako kwenye mazungumzo ya mwisho ya kumsajili kipa wa Jeunesse ya Ivory Coast, Vincent Atchouailou.
Kipa huyo aliyeibukia klabu ya vijana ya Rio Sport d’Anyama amewahi kuchezea Sawe Sports, msimu wa 2006/07 na Asec Mimosas, 2007/09.
Pia, amewahi kudakia timu ya vijana chini ya miaka 20 ya Ivory Coast katika mashindano ya Afrika nchini Benin mwaka 2005 na aliiwakilisha nchi yake katika Michezo ya Olimpiki, mwaka 2008.
Hata hivyo, usajili wachezaji hao wa kigeni utategemea uamuzi wa Kamati ya Utendaji ya TFF kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni wanaopaswa kusajili.
Kanuni za sasa ninataka wachezaji watano wa kigeni.

Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment