RAPA wa muziki wa kizazi
kipya, Khery Sameer ‘Mr Blue’, amesema anamshukuru mzazi mwenzake kwa kumfanya
aachane na matumizi ya bangi, pombe, sigara, mirungi na kuishi maisha ya
kawaida.
Akizungumza Dar es Salaam,Blue
alisema mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Wahyda, amemfanya aache kutumia
vilevi hivyo kutokana na kumwambia madhara yake.
“Alhamdulillahi nimeamka
salama nikiwa mwenye furaha, ahsante Mungu,na nashukuru pia kwa kufaulu mtihani
wa kuacha vilevi asante sana mke wangu Wahyda,” alisema.
Alisema anamshukuru
mpenzi wake kwa kufanikisha kuacha vilevi vyote bangi, sigara, mirungi, pombe
na kuishi kama binadamu wa kawaida.
Alitumia nafasi hiyo,
kuwashauri ndugu zake rafiki zake wa karibu wanaotumia vilevi hivyo kuachana na
matumizi ya vitu hivyo kwa ajili ya kukwepa kuharibiwa maisha yao.
0 comments:
Post a Comment