Wananchi hao wamekanusha
kauli ya Mbunge wa Kawe ,HALIMA MDEE aliyedai wamerubuniwa na kuuza
ardhi hiyo kwa bei poa.
Kauli hiyo ya wananchi imekuja baada ya mbunge huyo kutoa kauli za kulalamikia uuzwaji holela wa
ardhi ,ikiwemo ya vijiji hivyo bungeni wakati akichangia hoja katika Wizara ya
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya wananchi na viongozi wao
wamelaani kauli za baadhi ya wanasiasa
ambazo wakati mwingine
wamesema zina weza kuzua migogoro.
Akizungumzia hilo Meneja wa Bandari Mkoa wa Mtwara ,ABELI MWASENGA
amesema upimaji wa eneo waliotoa kwa ajili ya ujenzi wa bandari unaendelea
vizuri na mara utakapokamilika wanatarajia kutoa fidia kwa wakazi wa vijiji vya
Mgao na Kisiwa.
Kijiji cha mgano kimetoa ekari
1,500 wakati kijiji cha Kisiwa
kimetoa Ekari Elfu moja kwa ajili ya ujenzi wa bandari itakayomilikiwa na mwekezaji wa kiwancha cha saruji Al - Haji ALIKO DANGOTE.
0 comments:
Post a Comment