Mkurugenzi mtendaji wa
UNAIDS, Michel Sidibe' amesema kuwa dawa hizi ni mbadala wa zile ambazo
zilikuwa hazifurahiwi na watoto, zenye ladha mbaya.Dawa hizi zitawawezesha
watoto kuzidi kupata tiba nzuri na kuwafanya watoto wawe na afya, amesema
haikubaliki kuwa asilimia 24 pekee ya watoto walioathirika wapate dawa za
kupunguza makali.
Dawa hizi zimetengenezwa
nchini India, zina viambata vya Lopinavir na ritonavir ambazo zinaweza kuchanganywa
kwenye chakula cha mtoto.Dawa hizi haziharibiwi na joto la chakula na zina
ladha nzuri kuliko zinazopatikana sasa, vidonge hivi vinafaa kwa matibabu kwa
watoto.
Hii ni hatua mpya katika
mipango ya kuokoa maisha ya Watoto waishio na virusi vya ukimwi, Mkurugenzi wa
Mradi wa Ukimwi wa UNICEF,Craig McClure amesema '' tunatarajia kuimarisha
upatikanaji wa matibabu kwa ajili ya watoto wengi zaidi na kuunga mkono mpango
wa kuwafikia watoto wasiopata huduma hii duniani kote''.
0 comments:
Post a Comment