Image
Image

Wazee wanaogua kwa muda mrefu kwenye hospitali ya Mount Meru watelekezwa.


Baadhi ya wagonjwa wakiwemo wazee wenye maradhi  ya muda mrefu waliolazwa  kweny e  Hosipitali ya Mkoa  wa  Arusha  ya Mount  Meru wametelekezwa na ndugu  zao  baada ya  kutumia  rasilimali  zote  walizonazo  kugharamia  matibabu  bila  mafanikio.
Uchunguzi  uliothibitishwa  na  viongozi wa hosipitali hiyo  umebaini  kuwa  chanzo  ch a tatizo  hilo  ni umaskini  unaozikabili familia  wanakotoka  wagonjwa hao ambazo nyingi  ni  za  kipato  cha  chini na  zimeendelea  kukabiliwa  na  hali ngumu  kutokana  na  kugharamia  matibabu .
Tatizo hilo pia  limeelezewa  na  baadhi ya wasamaria  wema  wanaotembelea  wagonjwa katika  hosipitali  hiyo  ambao   licha  ya  kuelezea  ukubwa wa tatizo  wameiomba  serikali  na  jamii  hasa  watu  wenye uwezo kuangalia uwezekano  wa  kuweka  utaratibu wa  kusaidia  kundi  hilo.
Baadhi  ya  wagonjwa  wanaokabiliwa  na  matatizo hayo  pamoja  na  kuwashukur u watendaji wa  hosipitali  na wasamaria wanaowatembelea   wamesema  hali  ni  mbaya  kwani  baadhi  ya ndugu  wa  familia  wanakotoka   hawana  uwezo  wa  kununua  hata chupa  ya  maji  ya  kunywa   na  wengine  wanakosa  hata  nauli  ya  kufika hosipitali .


Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment