Kumbe sio tu wasanii wa bara la Afrika waliochukizwa na uandaaji na uendeshaji mzima wa shughuli za tuzo za BET, zilizofanyika jumapili ya june 28 mwaka huu kwamba hawakuwafanyia haki wanamuzi na washiriki kutoka Afrika, bali hata Rapa 50 Cents kutoka amerika hakuridhishwa na mwenendo mzima wa uandaaji wa tuzo za BET mwaka huu. Kilichomzingua na kumchanganya zaidi ni tuzo ya Mwgizaji bora wa kiume, “Best Actor” ambayo ilikwenda kwa “star” wa series ya Empire Terrence Howard.
Cents alipost Video Instagram, akieleza kushtushwa na tuzo hiyo kupewa Terrence bila hata kumtaja muigizaji Omari Hardwick aliyeigiza mara nyingi na kwa uwezo mkubwa ndani ya series hiyo.
“FOX bought the whole goddamn show. How you gonna have a Best Actor Award given to Terrence Howard and not even mention Omari Hardwick?” alilalama 50 kwenye video hiyo.
Katika maelezo mengine 50 alisema hakuridhishwa na kile alichokifanya P Diddy wakati akiperfom na kundi lake la Bad Boy, na kutoa maneno machafu akimdiss Diddy kwamba alifanya utumbo tu jukwaani.
0 comments:
Post a Comment