Image
Image

9 wafariki, 12 wajeruhiwa kwenye mapigano ya kikabila yaliyozuka nchini Sudan Kusini.


Watu 9 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine 12 kujeruhiwa kufuatia mapigano yaliyozuka kati ya jamii ya Panyon na Dhiei ambazo zinatokea katika kabila la Dinka.
Kwa mujibu wa taariifa za vyombo vya habari, mapigano hayo yalianza baada ya jamii ya Panyon kuishutumu jamii ya Dhiei kwa madai ya mauaji ya mtu wao mmoja.
Watu 5 kati ya wote waliofariki na majeruhi 7 walikuwa ni wa jamii ya Dhiei, ilhali wengine 4 kati ya waliofariki na majeruhi 5 walikuwa ni wa jamii ya Panyon.
Mapigano hayo yalisitishwa baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati na kujaribu kutatua mizozo.
Nchi ya Sudan Kusini imekuwa ikikumbwa na mapigano ya kikabila yaliyochochewa na mizozo ya kisiasa kati ya rais Salva Kiir na naibu wake wa zamani Riek Machar.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment