Image
Image

IMF yaahidi kuongeza msaada wa kifedha kwa nchi maskini zaidi Duniani.


Afisa mkuu wa Shirika la Fedha Duniani IMF, alitoa maelezo na kusema kwamba shirika hilo linapanga kuongeza misaada yake ya kifedha kwa kiwango cha asilimia 50 ili kusaidia nchi maskini kote duniani.
Hatua hiyo ilichukuliwa na IMF kama mojawapo ya mipango ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya mwaka 2015 iliyowekwa na UN.
Maelezo hayo yalibainishwa na mkurugenzi msaidizi wa IMF Zhu Min, aliyezungumza kwenye mkutano wa UN wa ufadhili na maendeleo uliofanyika katika mji mkuu wa Addis Ababa nchini Ethiopia.
Zhu alisema kwamba ajenda ya maendeleo ya UN inalenga kuboresha hali duni na kupunguza umaskini katika nchi zinazokabiliwa na maafa ya mara kwa mara yasiyoweza kuepukika.
IMF ilitangaza msaada huo siku chache baada ya mashirika mbalimbali ya kifedha na benki kadhaa kuahidi IMF ufadhili wa fedha zaidi ya dola bilioni 400 kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment