Apple Music yaweka rekodi mpya kwa kufikisha idadi ya wateja milioni 10.
Huduma mpya ya mauzo ya muziki mtandaoni ya Apple Music imepiga hatua kubwa muda mfupi baada ya kuzinduliwa.
Licha ya kuanzishwa hivi karibuni, Apple Music imefanikiwa kuweka rekodi mpya kwa kufikisha wateja milioni 10 ndani ya mwezi mmoja.
Apple Music ambayo bado inafanyiwa majaribio kabla ya kuzinduliwa kikamilifu, ilianzishwa kwa lengo la kukomesha wizi wa muziki mtandaoni unaorudisha nyuma mafanikio ya wasanii.
Kutokana na mafanikio hayo yaliyopatikana, Apple Music imeweza kuipiku Spotify yenye upinzani mkubwa katika soko la muziki mtandaoni.
Wateja hulipa fedha dola 9.99 kila mwezi ili kuweza kutumia huduma ya Apple Music mtandaoni.
0 comments:
Post a Comment