Habari kutoka kwa serikali ya Afghanistan zimefahamisha kifo cha aliyekuwa kiongozi wa Taliban, Mullah Omar amefariki.
Afisa wa serikali ya Afghanistan aliithibitisha kwa shirika la Anadolu kifo cha kiongozi wa Taliban Mullah Mohammad Omar.
Vyanzo vya habari viliripoti siku ya Jumatano kifo cha Mullah Omar, aliyekuwa kiongozi wa makundi ya kigaidi kati ya nchi ya Afghanistan na Pakistani.
Serikali ya Afghanistan ilitaka kutoa taarifa za kifo hicho siku ya Jumatano lakini wanachama wa Taliban hawakuwa tayari kutoa ushirikiano wao katika swala hilo.
Kifo cha kiongozi huyo kilitokea mara baada ya wawakilishi wa Afghanistan na Taliban kutarajia kufanya mkutano wa pili wa amani siku ya İjumaa.
0 comments:
Post a Comment