Mji huo wa China umeipiku mji pinzani wa Almaty ulioko Kazakhstan .
Beijing ambayo iliandaa mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 2008 ya msimu wa joto sasa umeingia katika daftari za kihistoria kwa kuwa mji mkuu wa kwanza kuandaa mashindano yote mawili ya Olimipiki ya msimu wa joto na yale ya msimu wa Baridi.
Kamati kuu ya kimataifa ya Olimpiki, ilikuwa ikikutana Kuala Lumpur,kupiga kura ya kuchagua mji upi kati ya Beijing au Almaty itakuwa mwenyeji wa mashindano ya olimpiki ya majira ya baridi mnamo mwaka 2022.
Ripoti kutoka Kuala Lumpur, mahala ambapo uamuzi huo umetolewa, inasema kwamba kamati hiyo ya IOC, iliamua kupiga kura kwa kutumia makaratasi baada ya kutokea matatizo ya kimitambo, katika shughuli za upigaji kura kielektroniki.
Mji huo mkuu wa China ni eneo zuri kwani lina uzoefu wa muda mrefu hasa baada ya kuandaa mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto, mnamo mwaka 2008.
Beijing ilikuwa ikijipigia debe ikisema kuwa kukosekana kwa barafu hakutakuwa na tatizo lolote.
Nao mji wa Almaty, nchini Kazakhastan, ulikuwa unaiomba kamati hiyo kuu ya kimataifa ya Olimpiki, kufanya maamuzi ya kina na kupigia kura jiji ambalo lenye barafu nyingi ardhini.
0 comments:
Post a Comment