Kwa mujibu wa maelezo ya NOCK,
fedha hizo zitatumika kugharamia mahitaji ya wanariadha 80 pamoja na timu mbili
za michezo tofauti.
Kenya inapanga kutuma timu ya mchezo
wa raga ya wanaume, na mojawapo kati ya timu ya taifa ya mpira wa wavu au ya
soka ya wanawake.
Mwenyekiti wa NOCK Kipchoge
Keino pia alitoa maelezo na kufahamisha kwamba wawakilishi kutoka nchini
wamezuru Brazil kwa lengo la kusaka uwanja mzuri wa mazoezi.
Akizungumza katika sherehe ya
uzinduzi wa shirika moja la misaada jijini Nairobi, Keino alisema, ‘‘Tuko
tayari kwa maandalizi ya timu zitakazowakilisha Kenya. Tunahitaji fedha
hizo kuanzia sasa ili kushughulikia wanariadha kati ya 80 na 100. ’’
Keino pia aliashiria mji wa Sao
Paolo kuwa kama eneo mwafaka la kukita kambi ya mazoezi kwa wanamichezo
wa Kenya kutokana na upungufu wa vifaa vya mazoezi katika mji wa Rio de
Janeiro.
Katika mashindano ya mwisho ya
olimpiki yaliyofanyika mjini London, Kenya ilituma jumla ya
wanariadha 51 na kushinda nishani 2 za dhahabu, 4 za fedha na 5 za shaba.
0 comments:
Post a Comment