Image
Image

Rais wa Zimbabwe amtunuku bondia Charles Manyuchi tuzo ya heshima.


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe, ametoa tuzo ya heshima kwa bondia Charles Manyuchi kutokana na mafanikio yake katika ulingo wa ndondi.
Tuzo hiyo kutoka kwa rais Mugabe iliyokabidhiwa Manyuchi siku ya Alhamisi, iliambatana na kitita cha fedha dola 50,000.
Wiki iliyopita, Manyuchi alifanikiwa kuzuia taji lake la shaba la WBC baada ya kumdondosha mpinzani wake Gianluca Frezza kutoka Italia kwenye pigano lililoandaliwa nchini.
Hapo awali, Manyuchi aliwahi kuilaumu serikali ya Zimbabwe kwa kutothamini mafanikio yake ambayo yalipewa umuhimu mkubwa zaidi katika nchi jirani ya Zambia.
Baada ya kilio ch amuda mrefu, hatimaye Manyuchi ameweza kuandaliwa sherehe ya tuzo katika ikulu ya rais, na kuahidi kuleta taji la fedha la WBC linaloshikiliwa na Amir Khan wa Uingereza.
Kwa tuzo hiyo, Manyuchi sasa ameweza kuingia kwenye orodha ya mashujaa wa michezo inayojumuisha muogeleaji Kirsty Coventry na mwanariadha wa marathon Steven Muzhingi walioiletea Zimbabwe nishani za olimpiki.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment