Image
Image

China kusaidia Kenya katika maboresho ya sekta ya viwanda.


Serikali ya China imeahidi kusaidia serikali ya Kenya kuboresha sekta ya viwanda ili kuimarisha uchumi wa nchi.
Balozi wa China nchini Kenya Liu Xianfa, alitoa maelezo hayo katika mkutano wa ujasiriamali uliofanyika katika mji mkuu wa Nairobi.
Akitoa hotuba yake katika mkutano huo ulioandaliwa chini ya usimamizi wa benki kuu ya China ICBC na CfC Stanbic Bank Kenya Limited, Liu alisema, ‘‘Serikali ya China ipo tayari kusaidia kuboresha sekta ya viwanda na kutoa taaluma ya kiufundi.’’
Mkutano huo ulihudhuriwa na wanabiashara zaidi ya 100 kutoka China na Kenya, pamoja na wawakilishi wa mashirika ya kifedha.
Katika kipindi cha miaka ishirini ya hivi karibuni, China imeibuka kuwa mojawapo ya washirika wakuu wa kibiashara wa nchi ya Kenya.
Takwimu za ubalozi wa China nchini Kenya zinaonyesha kwamba kiwango cha biashara kati ya nchi hizo mbili cha mwaka 2014 kimeongezeka kwa asilimia 53 ikilinganishwa na mwaka 2013 na kufikia dola bilioni 5.09.
Share on Google Plus

Kuhusu TAMBARARE HALISI

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment