Boko
Haram kimehusika na mauaji ya maelfu ya
watu pamoja na utekaji wa mamia ya wasichana.
Rais BUHARI
ameliambia Shirika la Associated
Press kuwa wapiganaji wa Boko Haram wataangamizwa katika kipindi cha miezi 18
au chini ya muda huo.
Hata
hivyo amekiri kuwa Serikali ya Nigeria haina taarifa za mahali walipo wasichana
waliotekwa katika Mji wa Chibok, Aprili mwaka jana na kuzua kilio kutoka jumuiya ya kimataifa.
Rais
BUHARI amesema Serikali yake ipo tayari
kuwaachia wapiganaji wa Boko Haram wanaoshikiliwa kwa kubadilishana na
wasichana waliotekwa, iwapo watawabaini
viongozi halisi wa kikundi hicho na kuwa na mazungumzo nao.
Rais
BUHARI aliyechaguliwa miezi miwili
iliyopita juzi amekutana na Rais BARACK OBAMA.
0 comments:
Post a Comment