Shirika la malipo kwa njia ya mtandao wa intaneti PayPal liliingia katika soko la hisa la Nasdaq kwa mara ya kwanza kama shirika huru tangu kunyakuliwa na shirika la eBay miaka 13 zilizopita.
Shirika la Paypal lilioanzishwa na Peter Theil lilinunuliwa na shirika la eBay kwa thamani ya dola bilioni 1.5 katika mwaka wa 2002.
Akiongea kuhusu utengano huu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Paypal Dan Schulman alisema, "Kama shirika linaloaminika zaidi duniani katika kusambaza fedha kwa njia ya kidijitali, tunafuraha kuorodheshwa katika soko la hisa." Schulman aliendelea kusema kuwa teknolojia ya sasa inabadilisha mfumo wa malipo na kufanya usafiri wa watu na usimamizi wa fedha zao kuwa rahisi na salama zaidi.
Kwa mujibu wa ripoti ya robo ya pili ya mwaka iliyotolewa na Schulman dola bilioni 66 zilisambazwa kupitia huduma ya Paypal huku shirika hilo likipata faida ya dola bilioni 2.3 hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.
0 comments:
Post a Comment